JamiiIran
Mlipuko mkubwa waitikisa bandari nchini Iran na kujeruhi 516
26 Aprili 2025
Matangazo
Mlipuko huo ulitokea katika bandari hiyo iliyopo nje kidogo ya kituo kikuu cha usafirishaji wa makontena cha Bandar Abbas huko Iran kinachoshughulikia karibu tani milioni 80 za bidhaa kwa mwaka.
Televisheni ya taifa ya Iran imeripoti kwamba, watoa huduma ya kwanza walikuwa wakijaribu kufika eneo hilo na wengine wakijaribu kuzihamisha bidhaa. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.