1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlipuko wa Ebola DRC: Visa 1003, vifo 254

23 Juni 2026

Maambukizi 1,003 ya Ebola yamerekodiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo mlipuko wa hivi karibuni umesababisha pia vifo vya watu 254.

Bunia I Maafisa wa afya wakivalia mavazi ya kujikinga na Ebola
Maafisa wa afya wakivalia mavazi ya kujikinga na Ebola huko DRCPicha: Benediction Murhabazi/AFP

Hii ni takwimu mpya iliyotolewa jana na taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Umma ya DRC (INSP) kufuatia mlipuko wa Ebola uliotangazwa Mei 15 mwaka huu.

Karibu visa vyote vya maambukizi  vimeripotiwa katika jimbo la Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini maeneo yanalokumbwa na migogoro ya makundi yenye silaha.

Virusi hivyo pia vimeenea hadi nchi jirani ya Uganda, ambapo Shirika la Afya Duniani WHO limerekodi visa 20 na vifo viwili, ingawa serikali mjini Kampala ilisema mapema mwezi huu kuwa ugonjwa umedhibitiwa. Mlipuko huu wa Ebola unaotokana na aina adimu ya virusi vya Bundibugyo ambayo haina chanjo au matibabu rasmi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW