1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Mlipuko wa lori la gesi waua 140 na kujeruhi wengi Nigeria

17 Oktoba 2024

Zaidi ya watu 140 wakiwemo watoto wamefariki dunia huko Nigeria baada ya lori la kusafirisha petroli lililokuwa limepindukia kulipuka, watu hao walipokuwa wakijaribu kuchota mafuta.

Ajali za malori yanayosafirisha mafuta nchini Nigeria hutokea mara kwa mara
Ajali za malori yanayosafirisha mafuta nchini Nigeria hutokea mara kwa maraPicha: Sani Maikatanga/AP/picture alliance

Wahanga wa mkasa huo waliangamia au kujeruhiwa walipokuwa wakijaribu kuchota mafuta. Haya ni kulingana na maafisa wa huduma za dharura Nigeria.

Dazeni kadhaa ya watu wamejeruhiwa. Maafisa wanasema idadi kubwa ya miili hiyo haiwezi kutambuliwa na kwamba karibu watu 140 wamezikwa katika kaburi la halaiki na kuna wengine waliozikwa katika maeneo mengine.

Mkuu wa huduma hizo za dharura Dokta Haruna Mairiga, amesema watu wengine wengi waliteketea na kugeuka majivu katika eneo la tukio.

Ajali za malori yanayosafirisha mafuta nchini Nigeria hutokea mara kwa mara, ajali ya hivi karibuni ikitokea katika jimbo la kaskazini la Jigawa katika mji wa Majiya.

Nigeria ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika na haina mfumo mzuri wa reli wa kusafirisha bidhaa hizo za mafuta.