Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg nchini Rwanda unapungua
18 Oktoba 2024Matangazo
Mlipuko wa virusi hatari vya Marburg nchini Rwanda unapungua baada ya chanjo kutolewa kwa watu walio hatarini zaidi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa afya. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa waziri wa afya wa Rwanda Sabin Nsanzimana na Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC. Mapema mwezi Oktoba,Rwanda ilianza kutoa dozi za chanjodhidi ya virusi vya Marburg ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa unaokaribiana na Ebola katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Katika hatua nyingine mkuu wa Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC Jean Kaseya amesema visa vipya vya ugonjwa wa Mpox vinaenea katika nchi nyingine za Afrika. Amesema idadi ya nchi zilizoathiriwa imeongezeka kutoka nchi sita mwezi Aprili hadi 18 mwezi Oktoba.