Mmarekani mwenye asili ya Kisaudi aachiwa huru Riyadh
21 Machi 2023Saad Ibrahim Almadi mwenye umri wa miaka 72 Mmarekani mwenye asili ya Kisaudi alikamatwa mnamo mwaka 2021 baada ya kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kile ambacho mwanawe amekiita ujumbe mwepesi kuhusu masuala kadhaa ikiwemo vita nchini Yemen na mauaji ya mwaka 2018 ya mwandishi habari wa Kisaudi Jamal Khashoggi.
Almadi ameachiwa huru ghafla hii leo kwa mujibu wa mwanawe Ibrahim aliyezungumza na shirika la habari la AFP akiwa nchini Marekani. Hata hivyo Almadi pia anakabiliwa na marufuku ya kutosafiri iliyowekwa mwaka jana na hivyo basi hawezi kuondoka nchini Saudi Arabia.
Kesi ya Almadi imeuongeza mvutano kati ya Riyadh na Washington,washirika wa muda mrefu ambao hivi karibuni wameonesha kutofautiana kuhusiana na masuala mbali mbali ikiwemo haki za binadamu.