1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mmoja auawa kwa mashambulizi ya Urusi mjini Lviv

19 Septemba 2023

Ukraine imesema mtu mmoja ameuawa kwenye mji wa Lviv, baada ya ndege isiyo na rubani ya Urusi kuyashambulia maghala matatu katika eneo la viwanda mapema leo asubuhi na kusababisha moto mkubwa.

Massive Angriffe auf ukrainische Stadt Lwiw
Picha: Roman Baluk/REUTERS

Gavana wa Lviv, Maxim Kozitsky, alisema maafisa wa zimamoto wanapambana kuuzima moto huo na kijana mmoja mwenye umri wa miaka 26 amepelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

Kozitsky alidai kuwa vikosi vya Urusi vilirusha ndege 18 zisizo na rubani ambapo 15 kati yao zilidunguliwa, zikiwemo saba zilizokuwa zimeushambulia moja kwa moja mji wa Lviv.

Soma zaidi: Urusi na Ukraine zahujumiana kwa droni na makombora

Wakati huo huo, serikali ya Ukraine ilisema meli ya mizigo iliyopakia nafaka ilikuwa imeondoka kwenye bandari ya Bahari Nyeusi, licha ya kitisho cha Urusi kwamba ingelizichukulia meli za kiraia kama za kijeshi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW