1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mnada wa matangazo ya TV ya Bundesliga waanza

Sekione Kitojo
8 Juni 2020

Chama kinachoendesha ligi ya Ujerumani Bundesliga DFL kimeanzisha mnada wa kuuza haki za kutangaza Bundesliga

Deutschland Augsburg | Bundesliga | FC Augsburg vs 1. FC Köln
DFL hupata asilimia 80 ya mapato kutokana na matangazo ya TVPicha: Reuter/M. Dalder

Mnada kwa  ajili ya haki za  kutangaza kwa njia  ya  televisheni  duru ya pili  ya  Bundesliga  unaanza  leo ambapo kitengo cha kinachoendesha  ligi ya  Ujerumani DFL kinatarajia  kukusanya mabilioni ya  dola  kutoka kwa watakaotoa  ahadi  mchakato  ambao utaendelea  hadi  Juni 17. Ligi  hiyo  inapata  zaidi  ya  asilimia 80 ya mapato  yake kuptia  matangazo  ya  televisheni  pamoja  na huduma za  matangazo ya  mtandaoni, ambapo huduma  hizo zimeingiza  kiasi  cha  euro bilioni 4.64 katika mapato ya  misimu minne  iliyopita  kwa  jumla. Mchakato  huo  ni  kwa  ajili  ya  msimu wa  mwaka  2021/22  hadi 2024/25.

Bayer Leverkusen ikipambana na Bayern Munich. Timu hizo zote zitacheza katika nusu fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Saabrucken na FrankfurtPicha: Reuters/M. Hangst

Michuano  ya  kombe  la  Ujerumani  linarejea  tena  uwanjani bila mashabiki  ambapo  michezo  ya  nusu  fainali  itapigwa kesho Jumanne  na  Jumatano. Bayer  Leverkusen inasafiri kwenda kuwakabili  Saarbruecken  ya  daraja  la nne, wakati Jumatano itakuwa  zamu  ya  Bayern Munich  kuoneshana  kazi  na  Eintracht Frankfurt  katika  marudio  ya  fainali  ya  mwaka  2018  ambapo Bayern  ilikubali  kipigo  cha  mabao 3-1.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW