Mnangagwa atuhumu wapinzani kuhusika na mripuko
27 Juni 2018Matangazo
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amelituhumu kundi la wapinzani ndani ya chama tawala cha ZANU-PF, lililokuwa likiunga mkono azma ya mke wa rais wa zamani Robert Mugabe, Grace ya kugombea urais, kwa kuhusika na mripuko wa bomu katika mkutano wa hadhara aliohudhuria wiki iliyopita.
Madai haya yametolewa wakati alipofanya mahojiano na shirika la habari la Uingereza, BBC. Hata hivyo, hakumtuhumu moja kwa moja bi. Grace kwa kuhusika na mpango huo, lakini alisema anatarajia kwamba wahusika watamatwa mara moja.
Watu wawili walikufa kufuatia mripuko huo, kwenye uwanja wa Bulawayo, wakati Mnangagwa alipokuwa akiondoka jukwaani baada ya kuwahutubia wafuasi wake.