1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Biashara na usafiri marufuku nyakati za sala

2 Septemba 2006

Waislamu wa siasa kali nchini Somalia hapo jana wamepiga marufuku biashara zote na usafiri wa umma wakati wa nyakati za sala katika maeneo yalioko chini ya udhibiti wao na hiyo kuzusha hofu utawala wa mtindo wa Taliban kuchukuwa madaraka katika nchi hiyo iliokosa utawala wa sheria.

Ikiwa ni siku moja kabla ya duru ya pili ya mazungumzo ya amani na serikali dhaifu ya Somalia huko Sudan masheikh wa Kiislam wameziamuru biashara zote zifungwe wakati wa nyakati tano za sala kila siku chini ya tishio la kuchukuliwa adhabu kali kutoka mahkama za Sharia za Kiislam.

Hatua hiyo inazidi kuimarisha utekelezaji wa sheria kali za Kiislam karibu katika eneo lote la kusini nchini Somalia na hiyo kuzidi kuipa changamoto mamlaka finyu ya serikali ya mpito na yumkini ikaongeza mvutano katika mazungumzo ya amani yanayodhaminiwa na Umoja wa Waarabu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW