1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Machafuko yaingia siku ya saba hii leo

24 Aprili 2007

Mashambulio ya makombora na mizinga yameukumba mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, kwa siku ya saba hii leo, huku wanajeshi wa Ethiopia wakiongeza kampeni yao ya kuwafurusha wanamgambo wa kiislamu na wapiganaji wa kimbari.

Baada ya usiku wa ufyatulianaji wa risasi, vifaru ya jeshi la Ethiopia vimeyashambulia maeneo ya kaskazini na kusini mwa Mogadishu katika juhudi za kuwadhoofisha wapiganaji ambao udhibiti wao wa mji mkuu huo umeizuia serikali ya mpito ya Somalia kufanya kazi mjini humo.

Mapambano makali yameripotiwa katika maeneo yanayoizunguka ikulu ya rais inayolindwa na majeshi ya Ethiopia na majeshi ya kulinda ya amani ya Umoja wa Afrika.

Mapigano pia yanaendelea katika eneo la Fagah kaskazini mwa Mogadishu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW