1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Maelfu walaani maadui wa Waislamu

12 Agosti 2006

Maelfu ya watu wenye kuunga mkono watawala wapya wa siasa kali za Kiislam wamefanya maandamano hapo jana katika mji mkuu baada ya sala ya Ijumaa wakitowa wito wa vita takatifu dhidi ya maadui wa Waislamu Mashariki ya Kati,Marekani na duniani kote.

Zaidi ya watu 2,000 walipiga mayowe ya Mungu Mkubwa na kulaani maadui wa Waislamu popote pale walipo.

Wengi wa waandamanaji wameilani Israel kwa dhima yake katika umwagaji damu uliodumu kwa mwezi mmoja sasa nchini Lebanon na pia kuishutumu jumuiya ya kimataifa kwa kubakia kimya wakati Lebanon ikishambuliwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW