MOGADISHU: Mripuko umeua watu 4 nchini Somalia
11 Februari 2007Matangazo
Mripuko uliotokea wakati wa sherehe za kijeshi katika mji wa bandari wa Kismayu nchini Somalia, umeua watu 4 na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa. Mashahidi wamesema,maafisa wa kijeshi wa ngazi ya juu na wajumbe wa polisi ni miongoni mwa wale waliojeruhiwa.Tangu vikosi vya serikali ya Somalia kuwatimua wanamgambo wa Kiislamu kwa msaada wa majeshi ya Ethiopia,Somalia inashuhudia mashambulio takriban kila siku.Serikali ya Somalia inaulaumu Muungano wa Kiislamu kuhusika na mashambulio hayo.Muungano huo ulidhibiti eneo la kusini mwa nchi kwa muda wa miezi sita kabla ya kutimuliwa majuma machache yaliopita.