1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU Mripuko wa bomu waua watu wawili mjini Mogadishu, Somalia.

17 Februari 2005

Watu wawili wameuwawa nchini Somalia kufuatia mripuko wa bomu mjini Mogadishu, wakati ambapo wajumbe wa umoja wa Afrika wamo mjini humo kutayarisha kupelekwa kwa walinda amani wa umoja huo. Walinda amani hao watakabiliwa na kibarua kigumu cha kuwasaidia viongozi wa serikali mpya ya Somalia walio uhamishoni mjini Nairobi, Kenya, kurudi Mogadishu. Wajumbe hao wa umoja wa Afrika walikuwa bado hawajafika mahala palipotokea mripuko huo. Inahofiwa kwamba kampeni za machafuko huenda zikaandaliwa kuwazuia viongozi hao wasirudi mjini Mogdishu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW