1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Ripoti kuwa Ethiopia imeingia ardhi ya Somalia

21 Julai 2006

Ripoti zinasema kuwa majeshi ya Ethiopia yameingia mji wa Baidoa nchini Somalia kuilinda serikali ya mpito ya Somalia iliyo dhaifu.Kuna khofu kuwa wanamgambo wa Muungano wa mahakama za Kiislamu huenda wakaishambulia serikali hiyo ya mpito katika makao yake mjini Baidoa.Mashahidi wanasema siku mbili za nyuma,wanamgambo hao waliujongea mji wa Buurhakana ulio karibu na Baidoa.Sasa lakini ripoti zasema wamerejea nyuma na wanamgambo wamekataa kuwa walitaka kuushambulia mji huo.Wakati huo huo katika mji mkuu wa Somalia,Mogadishu,mkuu wa ulinzi katika Baraza Kuu la Kiislamu la Somalia,ametoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kuishinikiza Ethiopia moja kwa moja kuondoka Somalia.