MOGADISHU: Shambulio la gruneti limesababisha vifo 3
2 Februari 2007Matangazo
Kwa mujibu wa serikali ya Somalia,si chini ya watu 3 wameua katika shambulio la gruneti lililotokea kwenye eneo la bandari katika mji mkuu,Mogadishu.Inasemekana kuwa wanamgambo wa Kiislamu ndio wanashukiwa kuhusika na shambulio hilo la gruneti.Hapo awali,watu mia kadhaa waliandamana mjini Mogadishu kupinga mpango unaotazamia kupeleka Somalia vikosi vya Kiafrika kulinda amani nchini humo.