1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Waislamu wa siasa kali wakutana na ujumbe wa Umoja wa Afrika na Ulaya

7 Julai 2006

Wanachama wa kundi la waislamu wenye siasa kali linaloudhibiti mji wa Mogadishu wamekutana na ujumbe wa Umoja wa Afrika, na maofisa wa Jumuiya ya nchi za kiarabu na Ulaya.

Ujumbe huo ulizuru nchini Somalia kutathimini hali ya usalama kabla wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika kupelekwa nchini humo.

Lakini viongozi wa mahakama za kiislamu wamesisitiza tena kwamba wanapinga hatua ya kuwapeleka wanajeshi wa kigeni kulinda amani nchini humo. Kundi hilo la kiislamu limeandaa maandamano kadhaa ya kupinga wanajeshi wa kigeni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW