1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Waislamu wataka kutambuliwa na madaraka

2 Septemba 2006

Vuguvugu lenye nguvu kubwa la Kiislam nchini Somalia linata kuheshimiwa na kushirikiana madaraka na serikali dhaifu ya mpito nchini humo wakati mazungumzo ya amani yanayodhaminiwa na Umoja wa Waarabu yakifunguliwa mjini Khartoum.

Huku kukiwa na matumaini ya kupunguza hali ya mvutano inayoongezeka ambayo inatishia kulidhoofisha zaidi taifa hilo lililokumbwa na machafuko Waislamu hao wa siasa kali wameepuka kutowa wito wa wazi wa kudai nyadhifa rasmi lakini wameweka wazi kwamba wanataka kutambuliwa.

Ujumbe wa Waislamu hao kwenye mkutano wa pili uliocheleweshwa mno kati ya pande hizo mbili umesema una haki ya kutawala taifa hilo lisilokuwa na utawala wa sheria lakini umekubali kutambuwa uhalali wa serikali ya mpito ikiwa kama ni ishara ya nia nje.