1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu yaandaa michuano ya soka

24 Januari 2024

Mji mkuu wa Somalia, Mogadishu unaandaa michuano ya soka katika uwanja wa michezo ambao kwa muda mrefu uligeuzwa na kuwa kambi ya jeshi kutokana na nchi hiyo kukumbwa na ghasia za wenyewe kwa wenyewe kwa miongo kadhaa.

Somalia | ufukwe Mogadishu
Moja ya fukwe za mji mkuu wa Somalia, MogadishuPicha: Mohamed Odowa/dpa/picture alliance

Mji huo mkuu Mogadishu, ni mwenyeji wa mashindano hayo ya kwanza ya soka katika miongo mitatu.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuwavutia maelfu ya watu.  Serikali ya Somalia kwa miaka mingi imefanya kazi ya kuurejesha kwenye hali nzuri uwanja huo wa taifa wa michezo wa mjini Mogadishu.

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Somalia Ali Abdi Mohamed, amesema uwanja huo uliofanyiwa marekebisho unakusudiwa kutimiza madhumuni yake ya asili, ambayo ni kuandaa mechi za mpira wa miguu.

Maoni yake yameungwa mkono na waziri wa michezo wa Somalia, Mohamed Barre, ambaye amesema madhumuni ya uwanja huo ni kuwajumuisha watu wenye maslahi sawa ambao ni wapenzi wa soka.  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW