Mogadishu,Bwana Gedi atembelea Somalia.
24 Februari 2005Matangazo
Waziri Mkuu wa Somalia aliyeuhamishoni Bwana Mohammed Ali Gedi leo amefanya ziara kwa mara ya kwanza nchini Somalia tangu aliposhika wadhifa huo mwaka jana na aliutembela mji ulio kaskazini mwa Mogadishu wa Jowhar.
Bwana Gedi pamoja na ujumbe wake kutoka Kenya ambako ndipo wanapoishi na kufanyia kazi za serikali kwa sasa,waliutembelea mji huo wakiwa wameanza ziara yao itakayowachukua siku tano ya kujionea wenyewe hali halisi ilivyo nchini Somalia.
Msemaji wa serikali ya Somalia Yusuf Baribari amethibitisha kuwa Bwana Gedi alikuwa mjini Jowhar na akasema kuwa Waziri Mkuu huyo na ujumbe wake pia watatembelea miji ya Beletuuein,Baidoa na Galkayo.Amesema Bwana Gedi hatotembela Mogadishu kwa sasa kutokana na usalama kuwa mdogo katika mji huo.