1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Meli ya Umoja wa mataifa yatekwa nyara na maharamia Somalia

26 Februari 2007

Maharamia wameteka nyara meli ya mizigo ya Umoja wa Mataifa katika pwani ya kaskazini mwa Somalia.

Meli hiyo MV Rozen ilitekwa nyara baada ya kupakua mizigo ya chakula cha msaada cha shirika la mpango wa chakula Duniani WFP katika eneo la Puntland.

Meli hiyo ilikuwa na wafanyikazi 12 wakati ilipotekwa nyara na hatma ya wafanyikazi hao ambao sita ni kutoka Sri-Lanka na sita ni wakenya haijulikani.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amefahamisha kwamba watekaji nyara hao hadi sasa hawajatoa matakwa yao.

Imetajwa kuwa meli hiyo imewahi kuepuka jaribio la kutekwa nyara mwaka jana.

Eneo la Pwani ya Somali ni mojawapo ya maeneo hatari kabisa duniani kutokana na maharamia wanaowinda kwenye eneo hilo ambalo halina walinzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW