1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Silaha zaendelea kuingia Somalia

15 Oktoba 2005

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeishutumu Somalia kwa kuendelea kukiuka vikwazo vya silaha vilivyoweka na Umoja huo miaka 13 ilyopita nchini humo.

Kwa mujibu wa mashahidi silaha zinaendelea kumiminika kimagendo nchini humo .Wakaazi wa vijiji vilivyoko karibu na mji wa Jowhar wamearifu kwamba malori mawili yaliyosheheni silaha yaliingia katika eneo hilo kutoka nchini Ethiopia hii leo.

Baadhi ya wakazi hao wamedai kwamba silaha hizo zinamilikiwa na rais wa mpito nchini Somali Abdullahi Yusuf ambaye ameweka ngome yake mjini Jowhar baada ya kupinga serikali yake kuwekwa mjini Mogadishu.

Hata hivyo kambi ya rais Yusuf haikuweza kufikiwa mara moja kueleza juu ya madai hayo lakini baadhi ya maofisa kwenye serikali mpya awali walisikika wakisema hadharani juu ya juhudi zao za kuunda jeshi na vikosi vya usalama kusaidia kuweka amani nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW