1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mohammed al-Bashir kiongozi wa mpito Syria

10 Desemba 2024

Aliyekuwa mkuu wa serikali katika ngome ya waasi ya Idlib, kaskazini-magharibi mwa Syria, Mohammed al-Bashir amejitangaza kuwa ataongoza kipindi cha mpito cha serikali ya Syria hadi Machi mwaka 2025.

Syrien | Mohammed al-Bashir
Mohamed Bashir, akiwa na waandishi wa habari katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria Novemba 28, 2024.Picha: Omar Haj Kadour/AFP/Getty Images

Hatua hiyo inatekelezwa katika kipindi ambacho serikali ya Israel ikikanusha  wanajeshi wake kufanya mashambulizi katika eneo lisilokuwa na shughuli za kivita la Syria.

Uamuzi wa Bashir unafuatia kuondolewa madarakani kwa rais Bashar al-Assad. Awali Jumatatu, vyombo vya habari vya mataifa ya Kiarabu viliripoti kwamba al-Bashir alikuwa amepewa jukumu la kuunda serikali mpya ya Syria baada ya mkutano wa viongozi wake wakuu.

Mkutano mwingine muhimu ulifanyika leo katika hoteli moja mjini Damascus, uliongozwa na kiongozwa na mkuu wa muungano wa waasi, Ahmed al-Sharaa  aliefahamika pia kwa jina Abu Mohammed al-Joulani  ulijumuisha mawaziri wa serikali iliyopita.

Uongozi wa mpito utadumu hadi Machi

Katika hotuba fupi kwenye televisheni ya serikali, Mohammed Bashir, mtu ambaye hajulikani sana katika sehemu kubwa ya Syria amesema ataongoza mamlaka ya muda hadi Machi Mosi.

Watu wakitembea karibu na sanamu huko Damascus, baada ya waasi wa Syria kumwondoa madarakani Rais Bashar al-Assad, Syria Desemba 10, 2024.Picha: Mahmoud Hassano/REUTERS

Nyuma yake kulikuwa na bendera mbili. Kijani, nyeusi na nyeupe iliyopeperushwa na wapinzani wa Assad katika muda wote wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, na bendera nyeupe ya kiapo cha imani ya Kiislamu katika maandishi nyeusi, ambayo kwa kawaida hutumiwa huko Syria na wapiganaji wa Kiislamu wa madhehenu ya Sunni.

Recep Erdogan ambae ni Rais wa Uturuki ameipongeza hatua hiyo,"Kuanzia sasa, hatuwezi kuruhusu Syria igawanywe tena. hatuwezi kamwe kuruhusu eneo la nchi kuwa uwanja wa vita tena. Shambulio lolote dhidi ya uhuru wa watu wa Syria, uthabiti wa serikali mpya ya Syria, na uadilifu wa eneo la kale la Syria tutalishughulikia  pamoja na watu wa Syria." Alisema kiongozi huyo wa Uturuki.

Kurejea kwa hali ya kawaida Damascus

Katika mji mkuu wa Syria, benki zilifunguliwa kwa mara ya kwanza tangu kupinduliwa kwa Assad. Maduka pia yalikuwa yakifunguliwa tena, idadi kubwa ya magari lirejea barabarani, mafundi ujenzi waliendelea na shughuli zao za marekebisho na ukarabati katikati mwa jiji la Damascus pamoja na wasafisha mitaa waliingia kazini.

Kunaelezwa pia kupungua kwa idadi ya watu wenye silaha mitaani. Vyanzo viwili vilivyo karibu na waasi vilisema kulitolewa amri ya wapiganaji kuondoka mijini na polisi kwa ajili ya usalama wa ndani wa kawaida  kutoka katika kundi kuu la waasi, Hayat Tahrir al-Shams (HTS)  wakapelekwa katika maeneo hayo.

Hatua ya kurejesha hali ya kawaida inatekelezwa licha ya kuwepo kwa hali mbaya ya mashambulizi ya anga kutoka Israel, yakilenga kambi za kijeshi za jeshi la Syria, ambalo vikosi vyake vimetoweka kutokana na nguvu ya kusonga mbele kwa wapiganaji waliomuondoa Assad.

Soma zaidi:Israel yafanya mashambulizi makubwa nchini Syria

Israel, ambayo imeripotiwa kutuma vikosi kuvuka mpaka katika eneo la Syria imesema mashambulizi yake ya anga yalilenga katika kuzuia silaha zisiangukie kwenye mikono yenye uadui. Na imekanusha ripoti kuwa vikosi vyake vilikuwa vimesonga mbele zaidi ya eneo lisilokuwa na shughuli za kijeshi la Syria na kufanya mashambani kusini magharibi mwa Damascus.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW