1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Sudan: Hospitali nyingine yashambuliwa El-Fashir

24 Juni 2024

Moja ya hospitali zilizosalia na zinazofanya kazi katika mazingira magumu kwenye mji wa el-Fashir nchini Sudan imeshambuliwa kwa risasi huku mhudumu mmoja wa afya akiripotiwa kuuawa Ijumaa jioni.

Hospitali inayomilikiwa na Shirika la Madaktari wasiona mipaka MSF huko El-Fasher, Sudan
Hospitali inayomilikiwa na Shirika la Madaktari wasiona mipaka MSF huko El-Fasher, SudanPicha: ALI SHUKUR/AFP

Taarifa hii imetolewa hapo jana mjini Geneva, Uswisi na Shirika la Madaktari wasio na mipaka MSF ambao wameongeza kuwa hali katika jiji hilo ilikuwa mbaya mno na msaada dharura haukuweza kutolewa.

Soma pia: Baraza la usalama la umoja wa mataifa lataka kusitishwa kwa mzingiro El-Fasher

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamekuwa wakiripoti mashambulizi ya mara kwa mara yanayozilenga hospitali huko al-Fashir huku maduka yakiporwa na wanawake wakifanyiwa ukatili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW