1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moldova yapiga kura kuhusu mustakabali wa Umoja wa Ulaya

Hawa Bihoga
3 Novemba 2024

Moldova imefanya duru ya pili ya uchaguzi wa rais, ikiwa ni muhimu kuamua mwelekeo wake kati ya Ulaya na Urusi, huku kukiwa na hofu ya kuingiliwa na Urusi.

Uchaguzi Moldova 2024 | Maia Sandu
Rais wa sasa, Maia Sandu akipiga kuraPicha: Vladislav Culiomza/REUTERS

Hapo awali ya kura ya maoni ambayo ilionyesha ushindi wa asilimia 50.35 kwa upande unaopendelea Umoja wa Ulaya. 

Rais wa sasa, Maia Sandu, alipata asilimia 42.5 katika duru ya kwanza, huku Alexandr Stoianoglo, anayeungwa mkono na Urusi, akipata asilimia 26. 

Sandu alilaumu uingiliaji wa kigeni kwa matokeo finyu ya kura ya maoni na alidai polisi iligundua mpango wa Urusi wa kununua kura. Katika siku ya uchaguzi, alisisitiza umoja ili kulinda uhuru na kuonya dhidi ya kununua kura.

Soma pia:Moldova yaridhia kwa wingi mdogo kujiunga na EU

Mamlaka ziliripoti ongezeko la vitisho kwa wapiga kura, huku Waziri Mkuu Dorin Recean akisema hali hiyo ni jaribio la kuleta hofu. 

Ingawa wagombea wote wanadai kuunga mkono EU, Stoianoglo, ambaye alikataa kura ya maoni, anapigia upatu sera ya usawa katika siasa za kigeni, jambo ambalo linaweza kukwamisha malengo ya Moldova kujiunga na Umoja wa Ulaya iwapo atashinda.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW