1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA: Ellen Johnson-Sirleaf aendelea kuongoza uchaguzi wa Liberia

10 Novemba 2005

Waziri wa fedha wa zamani, Ellen Johnson-Sirleaf, anaendelea kuongoza katika matokeo ya uchaguzi nchini Liberia. Maofisa wa tume ya uchaguzi wamesema Sirleaf anaongoza kwa asilimia 57.9, huku mpinzani wake mwanasoka mashuhuri George Weah, akiwa na asilimia 42.1.

Tume ya uchaguzi itachunguza madai yote ya udanganyifu yaliyotolewa na Weah. Kiongozi wa tume ya kulinda amani ya umoja wa mataifa nchini Liberia amesema uchaguzi huo ulifanyika kwa amani na haukuwa na udanganyifu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW