MONROVIA: Mapigano yaendelea kaskazini mashariki mwa Liberia
6 Januari 2004Matangazo
Habari kutoka mji mkuu wa Liberia - Monrovia, zinasema mapigano makali yamekua yakiendelea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwenye mpaka na Ivory Coast, baina ya makundi ya wanamgambo watiifu kwa Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor, na waasi wa chama cha Model.
Kwa mujibu wa Redio moja ya kanisa katoliki Veritas, nyumba nyingi zimechomwa moto na mali kuibiwa; lakini redio hiyo haijasema ikiwa idadi ya waliofariki au kujeruhiwa imejulikana.
Kwa mujibu wa habari hizo, mapigano yalizuka, pale waasi wa chama cha Model walipotaka kujiingiza katika eneo linalodhibitiwa, tangu mwezi ogasti mwaka jana, na wanamgambo watiifu kwa rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor.
Mwezi Ogasti mwaka jana makundi mbali mbali ya waasi na vyama vya kisiasa vya Liberia kumi na vinane, walisaini makubaliano ya kusitisha mapigano, na kushiriki katika serikali ya mpito, inayoongozwa na Bwana Gyude Bryant.