1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA: Weah aongoza katika uchaguzi Liberia

16 Oktoba 2005

Matokeo ya awali katika uchaguzi wa rais nchini Liberia yanaonyesha kwamba aliyekuwa mwanasoka maarufu George Weah anaongoza kwa asilimia zaidi ya 26.4

Mgombea mwingine mwenye matarajio makubwa bibi Ellen Johson Sirleaf anafuatia akiwa na asilimia 15.2

Matokeo hayo yanatokana na theluthi moja ya kura zilizohesabiwa katika vituo alfu tatu vya kupigia kura.

Wajumbe wa kimataifa wanaofuatilia uchaguzi huo wamesema kwamba umefanyika katika hali ya utulivu.

Watu 22 wamesismama katika uchaguzi huo kugombea kiti cha urais.

Iwapo hapatakuwa na mgombea atakaepata kura zaidi ya asilimia hamsini, raundi ya pili itafanyika baina ya wagombea wawili watakaoongoza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW