MONROVIA:Mgombea rais wa kike aongoza Liberia
12 Novemba 2005Nchini Liberia,wafuasi wa mgombea urais George Weah wamepambana na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa,baada ya matoeko rasmi ya uchaguzi kuonyesha kuwa anashindwa.Vikosi vya Umoja wa Mataifa vilifyatua mabomu ya kutoa machozi,mamia ya watu walipoandamana katika mji mkuu Monrovia wakilalamika kwamba uchaguzi ulikuwa na udanganyifu.Weah aliekuwa nyota ya kabumbu aliwaomba wafuasi wake wapokee kwa amani habari za kushindwa kwake.Wakati asilimia 97 ya kura zimehesabiwa,mchumi wa zamani wa Benki ya Dunia,Bibi Ellen Johnson-Sirleaf amejisombea kiasi ya asilimia 60 ya kura.Bibi Johnson-Sirleaf anatarajiwa kuwa kiongozi wa kwanza wa kike aliechaguliwa na wananchi barani Afrika. Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa wamesema uchaguzi uliofanywa siku ya jumanne,kwa jumla ulikuwa huru na wa haki.