MONROVIA:Wapiganaji wasalimisha silaha
8 Desemba 2003Matangazo
Nchini Liberia mamia ya wapiganaji wa serikali wakiwemo watoto wamekabidhi silaha zao katika kituo cha kusalimisha silaha cha Umoja wa Mataifa. Lakini katika kile kinachoelezwa kuwa kama bahati mbaya wapiganaji wengi zaidi wanagoma kusalimisha silaha zao kwa kusema kwamba walikuwa wakitarajia kupatiwa fedha zaidi kwa ajili ya kubadilishana na silaha hizo.Wapiganaji wanaojiunga na mpango huo wa kusalimisha silaha watapatiwa dola 300 pamoja na mafunzo ya kikazi lakini kwanza wataweza tu kupatiwa dola 150 mwishoni mwa mpango huo wa wiki tatu wa kusalimisha silaha.