1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA:Weah aongoza katika uchaguzi wa Liberia

15 Oktoba 2005

Yadhihirika kuwa mcheza mpira mashuhuri wa zamani George Weah,anawapita wagombea kura wengine 21 katika matokeo ya uchaguzi wa kwanza kupata kufanywa nchini Liberia tangu kumalizika kwa vita nchini humo.Ellen Johnson Sirleaf aliekuwa mtaalamu wa uchumi wa Benki Kuu ya Dunia,ni mshindani wake mkuu.Kuna uwezekano wa kufanywa duru ya pili ya uchaguzi kwa sababu Weah bado hajakaribia uwingi unaohitajiwa kuwa mshindi pekee.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeisifu Liberia kwa uchaguzi uliofanywa kwa amani.Baraza hilo limesema,utaratibu huo wa uchaguzi huenda ukawa hatua muhimu sana ya kurejesha amani katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi,ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe vilimalizika mwaka 2003.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW