1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONUSCO: Kuna ongezeko la ukiukaji wa haki DRC

26 Novemba 2025

Ripoti ya kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Kongo MONUSCO inaonesha kuna ongezeko la ukiukaji wa haki za binadamu.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa, MONUSCO
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa, MONUSCOPicha: Jospin Mwisha/AFP

Kitengo cha MONUSCO kimeyasema haya katika chapisho lake la taarifa yake ya miezi sita ya kwanza ya mwaka 2025 kuhusu haki za binaadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Taarifa hiyo inaonesha ongezeko la asilimia 11 la ukiukaji wa haki za kibinadamu na ongezeko la asilimia 12 la waathirika ikilinganishwa na miezi sita ya mwaka jana.

Takwimu zinawakilisha zaidi ya asilimia 100

Taarifa ya ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa inabainisha visa kadhaa vya ukiukajiwa haki za binadamu na unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro, vilivyotekelezwa dhidi ya waathirika 266, wakiwemo wanawake 264 na wanaume wawili katika majimbo sita ya Kongo.

Walinda amani wa MONUSCO Jamhuri ya Kidemokrasi ya KongoPicha: AFP via Getty Images

Ofisi hii inaonyesha kuwa takwimu hizi zinawakilisha zaidi ya asilimia 100 ya waathirika ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2024, ambapo janga hili liliwahusisha waathirika 156, wakiwemo wanawake 155 na mwanaume mmoja.

Taarifa hiyo inaonyesha kuwa kesi nyingi zilirekodiwa, wakiwemo waathiriwa 115 katika Jimbo la Kivu Kaskazini, ikifuatiwa na jimbo la Ituri lenye waathiriwa 97, Jimbo la Kivu Kusini na waathiriwa 41, na Jimbo la Maniema lenye waathiriwa 12. Lakini pia, mwathirika mmoja alirekodiwa katika Jimbo la Tanganyika.

Katika Jimbo la Kivu Kusini, baadhi ya watetezi wa haki za kibinadamu wameelezea kuwa wanaishi katika hofu iwe katika upande unaodhibitiwa na makundi yenye silaha, au katika upande unaodhibitiwa na Serikali Kuu ya Kinshasa.

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu umeongezeka kwa asilimia 21 katika Jimbo la Ituri, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Makundi yaliyojihami yanachangia kueneza ghasia

Takwimu hizo zinaonesha kwamba kundi la waasi la ADF linaloshirikiana na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu, IS, lilihusika na visa 198 vya ukiukaji wa haki za binadamu huko Ituri na Kivu Kaskazini, na waathiriwa wasiopungua 1,071, katika miezi sita ya kwanza ya mwaka pekee.

Makamanda wa kundi la wanamgambo wa CODECOPicha: ALEXIS HUGUET/AFP

Lakini pia makundi ya CODECO, Zaire, CRP na CNLC yanayonyoshewa kidole yakihusishwa kuchangia katika kusambaza ghasia jimboni Iruti na Kivu kaskazini, na AFC/M23 katika majimbo ya Kivu kaskazini na Kivu Kusini.

Muungano wa AFC/M23 unaandaa mkutano na waandishi haari leo mjini Goma ili kuangazia masuala yakibinadamu katika maeneo yaliyo chini ya utawala wake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW