MONUSCO:Haipo tayari kukabiliana na M23
14 Julai 2022Wakati wa mkutano na waandishi wa habari jana Jumatano mjini Kinshasa, Monusco ilieleza kuwa M23 wanajiendesha kama jeshi la kawaida na wana vifaa vya kijeshi vya hali ya juu kabisa.
Jeshi la Umoja wa Mataifa hapa nchini Kongo bado halijaelewa ni vipi kundi la waasi linaweza kuwa na zana za kijeshi zinazozidi hata zile za jeshi la kawaida.
Wengi wanasalia na swali la msingi kwamba vikosi vya jeshi la taifa la Kongo na vile vya Monusco havina uwezo wa aina hiyo?
Msemaji wa MONUSCO Mathias Gillman, ameviambia vyombo vya hababro DRC kwamba vifaa walivyonavyo ni kwa ajili ya kukabiliana na vikundi vinavyomiliki silaha pamoja na wanamgambo ila sio dhidi ya majeshi ya kawaida yenye nguvu.
Soma pia:DRC: Wabunge waeleza mashaka yao juu ya kuongezeka wanajeshi
"Wasiwasi wetu ni kwamba ikiwa hali hiyo ya M23 itaendelea, itavuruga sana usalama katika maeneo ambayo ADF na Codeco pamoja na Mai-Mai wanaendesha harakati zao." Alisema msemani wa MONUSCO Mathias
MONUSCO ikijinasua ADF yaendeleza mauaji ya raia
Wakati huko Rutshuru mkoani Kivu Kaskazini jeshi la Kongo linakabiliana na waasi wa M23 ambaoserikali ya Kongo inawataja kuwa magaidi, upande mwengine waasi wa ADF wanaendeleza mauaji dhidi ya raia katika eneo la Beni huko huko Kivu Kaskazini.
Watu saba waliuawa na waasi hao usiku wa kuamkia Jumatano huko Paida wakati waasi walitaka kushambulia gereza la Kangwayi.
Shambulizi hilo lilifanyika karibu ya makao makuu ya sekta ya operesheni za kijeshi hiiyo ikitajwa na wataalamu kuwa ni mbinu ya adui ili kuchanganya upande wa mashambulizi.
Soma pia:Mwakilishi Maalum wa katibu mkuu wa UN afanya ziara DRC
Kapteni Antony Mualushay, msemaji wa Operesheni Sokola 2 ameiambia DW kwamba adui hawezi kupambana na vikosi vya makao makuu, lakini alitaka kuzuia askari kusaidia kwenye gereza.
"Ndio maana adui alitumia makundi mawili, moja ya kuwavuruga watu waliokuwa Bulongo na kundi jingine kuzuia askari waliokuwa karibu na gereza kusaidia kwenye gereza la Kangwayi." Alisema
Yote hayo yamejiri huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikijiandaa kwa uchaguzi wa 2023, ila baadhi ya wachambuzi wanahofia kuvurugwa kwa mchakato wa uchaguzi huo.