1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morgan Tsvangirai arudi nyumbani

24 Mei 2008

-

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Demokratic Change MDC nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini alikokuwa akiishi kwa muda.Tsvangirai amechukua hatua hiyo kwa ajili ya kujitaarisha kuanza kampeini ya duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya rais Robert Mugabe licha ya hofu kwamba kuna njama za serikali za kutaka kumuua kiongozi huyo wa upinzani.Wiki iliyopita Tsvangirai alifutilia mbali safari yake ya kurudi Zimbabwe kufuatia tetesi kwamba kuna njama za serikali za kumuua lakini serikali ilikanusha na kudai kwamba ni propaganda za chama cha MDC.Aidha alipowasili katika uwanja wa ndege mjini Harare Tsvangirai amepinga uwezekano wa kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa na akaapa kwamba atamshinda rais Mugabe katika duru ya pili ya uchaguzi. Tsvangirai amekuwa akisafiri katika nchi mbali mbali tangu mwezi Aprili 8 kujaribu kutafuta uungaji mkono wa kimataifa wa kumshinikiza Mugabe aachie madaraka baada ya uchaguzi wa mwezi Marchi 29 ambao anadai alimshinda rais huyo.Chama cha MDC kimeitaka jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC kuwa tayari kupeleka waangalizi wake katika uchaguzi huo wa mwezi ujao.