1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morgan Tsvangirai arudi Zimbabwe

24 Mei 2008

-

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Demokratic Change Mdc Morgan Tsvangirai yuko njiani kurudi nchini mwake kwa ajili ya kuanzisha kampeini ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais.Kiongozi huyo wa chama cha MDC ambaye alikuwa anaishi kwa muda nchini Afrika Kusini amefahamisha kuwa anafurahia kurudi nchini Zimbabwe licha ya hofu kwamba kuna njama za kutaka kumuua.Msemaji wa chama hicho ameeleza bado kuwa wasiwasi juu ya suala la usalama kwasababu ya ghasia zinazoendelea Zimbabwe lakini mgombea wao yaani Morgan Tsvangirai hana budi na amepania kuanza kampeini ya uchaguzi wa tarehe 27 mwezi ujao dhidi ya rais Robert Mugabe