1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morgan Tsvangirai autaka Umoja wa mataifa kuingilia mgogoro Zimbabwe

22 Aprili 2008

-

ACCRA

Kiongozi wa Upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefanya mazungumzo hapo jana na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon na kuutolea mwito umoja huo pamoja na Umoja wa Afrika kuingilia kati mgogoro wa kisiasi unaoikumba nchi yake.Tsvangirai amemwambia katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kwamba anahisi juhudi za nchi za kiafrika za kujaribu kuishawishi tume ya uchaguzi na serikali ya Zimbabwe kutangaze matokeo ya uchaguzi hazijapiga hatua.Tsvangirai ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Demokratic Change MDC anaamini kwamba amemshinda rais Mugabe katika matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika zaidi ya wiki tatu zilizopita.Kwengineko makundi ya haki za binadamu nchini Zimbabwe yamesema yamegundua makambi ambako watu waliopigia kura chama cha MDC wanateswa lakini serikali imekanusha madai hayo.Wakati huohuo shughuli ya kuhesabu upya kura katika majimbo 23 kati ya 210 ambayo ilitazamiwa kukamilika jana imecheleweshwa kutokana na sababu ambazo hazijulikani.Kwa mujibu wa katibu mkuu wa chama cha MDC Tendai Biti ghasia za baada ya uchaguzi wa Zimbabwe zimesababisha watu elfu 3000 kuachwa bila makaazi wengine 500 wamejeruhiwa na 10 kuuwawa.