Morocco: Muungano tawala washindwa pakubwa katika uchaguzi
9 Septemba 2021Matangazo
Katika kikao na waandishi wa habari, waziri wa masuala ya ndani wa Morocco Abdelouafi Laftit amesema chama cha Haki na Maendeleo - Justice and Development, PJD, ambacho kilikuwa kinaongoza muungano uliokuwa unatawala kwa mwongo mmoja, kimeshuhudia uungwaji mkono wake bungeni kuporomoka kutoka viti 125 hadi viti 12 tu.
Mahasimu wake chama cha National Rally of Independents RNI kimenyakua viti 97 huku chama cha Authenticity and Modernity Party PAm kikipata viti 87 nacho chama cha Istiqlal kikiambulia viti 78 katika bunge lenye jumla ya viti 395.
Chama cha RNI ambacho kilikuwa chama kidogo katika muungano tawala, kinaongozwa na mfanyabiashara bilionea nchini humo Aziz Akhannouch.