JamiiMorocco
Morocco yaanza kutoa fedha kwa familia za watu wasiojiweza
26 Desemba 2023Matangazo
Tangazo hilo limetolewa na Waziri Mkuu wa Morocco, Aziz Akhannouch, ambaye amesema wanufaika wa mpango huo watapokea kila mwezi kuanzia kiasi dirham 500 ambazo ni sawa na dola 50 za Marekani.
Akhannouch amesema malipo ya kwanza chini ya mpango huo mpya wa taifa yatafanyika siku ya alhamisi wiki hii.
Mpango huo uliopendekezwa muongo mmoja uliopita ni sehemu ya mageuzi mapana ya utoaji huduma za jamii yaliyotangazwa na Mfalme Mohammed VI mnamo mwaka 2020.
Ajenda yake ya mageuzi ilijumuisha pia tangazo la mwaka 2021 la kuanza kutolewa bure kwa huduma za msingi za afya kwa raia wote wa Morocco.