1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morocco yatinga hatua ya 16 Bora AFCON

30 Desemba 2025

Morocco, wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), wamefuzu hatua ya 16 bora baada ya kuifunga Zambia mabao 3-0 na kuongoza Kundi A.

AFCON | Egypt fans waving flags during Angola vs Egypt at AFCON in Agadir
Mashabiki wa Misri wakitazama kandanda katika uga wa Agadir Morocco.Picha: Franck Fife/ AFP

Ushindi huo unaipa Morocco faida ya kuendelea kucheza mechi zake za mtoano katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, wa mjini Rabat, wenye uwezo wa mashabiki karibu 70,000, ambao pia utatumika kwa fainali ya AFCON Januari 18.

Kwa mujibu wa kanuni za AFCON, timu mbili bora kutoka kila kundi pamoja na timu nne bora zilizomaliza nafasi ya tatu zinafuzu hatua ya 16 bora.

Timu zilizofuzu kupitia nafasi ya tatu ni:

Kundi D: Senegal, Kongo, Benin

Kundi F: Ivory Coast, Cameroon, Msumbiji

Kundi E: Burkina Faso, Sudan (pamoja na Algeria)

Angola bado ina nafasi ya kufuzu iwapo Nigeria itaifunga Uganda na Tunisia kuichapa Tanzania katika Kundi C.

Rabat yashangilia ushindi wa Morocco

Baada ya ushindi huo, mji wa Rabat ulitawaliwa na shangwe kubwa, mashabiki wakipiga honi, kupeperusha bendera na kupuliza vuvuzela. Hali hiyo ilitofautiana na mechi iliyopita ambapo wachezaji walizomewa na mashabiki, hali iliyomlazimu nahodha Achraf Hakimi kutoa onyo.

Wachezaji wa Moroko washerehekea ushindi katika michuano ya AFCON.Picha: Fareed Kotb/Anadolu/picture alliance

Ayoub El Kaabi alifunga bao la kuvutia kwa bicycle kick dakika ya 50, ambalo lilithibitishwa na VAR baada ya awali kuonekana kama ameotea. Ashraf Hakimi aliingia uwanjani dakika ya 64, ikiwa ni mara yake ya kwanza katika AFCON hii baada ya kupona jeraha la kifundo cha mguu.

Matokeo mengine AFCON

Katika mechi nyingine ya Kundi A, Mali ilitoka sare tasa dhidi ya Comoros na kumaliza nafasi ya pili. Kocha Tom Saintfiet alieleza wasiwasi kuhusu kiwango cha kikosi chake kuelekea hatua ya mtoano.

Afrika Kusini ilipata ushindi muhimu wa 3-2 dhidi ya Zimbabwe na kumaliza nafasi ya pili Kundi B nyuma ya Misri. Misri ilicheza bila nyota wake wakuu akiwemo Mohamed Salah, baada ya kocha Hossam Hassan kuwapumzisha kwa maandalizi ya hatua ya mtoano.

Afrika Kusini sasa inasubiri kukutana na mshindi wa pili kutoka Kundi F—Ivory Coast, Cameroon au Msumbiji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW