1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Kiongozi wa waasi wa Chechnya auwawa

10 Julai 2006

Kiongozi wa waasi nchini Chechnya Shamil Basayev, ameuwawa na wanajeshi wa Urusi.

Shirika la habari nchini Urusi, Interfax, likimnukulu kiongozi wa idara ya ujasusi nchini humo, FSB, limesema Basayev alikuwa mwanamume aliyeafutwa sana nchini Urusi.

Basayev analaumiwa kwa mashambulio kadha wa kadha katika muongo mmoja uliopita.

Inasemekana Basayev aliuwawa katika oparesheni ya usiku wa kuamkia leo iliyofanywa na vikosi maalumu vya Urusi katika mkoa wa Ingushetia, kusini mwa Caucasus, unaopakana na Chechnya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW