1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Maskhadov auawa Chechnia

9 Machi 2005

Kiongozi wa waasi wa Kichechnia,Aslan Maskhadov ameuawa.Msemaji wa Russia amearifu kuwa Maskhadov aliuawa katika opresheni maalam ya jeshi katika kijiji kimoja cha Chechnia.Mjumbe wa Chechnia mjini London amethibitisha kuwa maiti iliyoonyeshwa kwenye televisheni ya Russia ilikuwa ya kiongozi huyo wa waasi.Maskhadov aliekuwa na umri wa miaka 53 alichaguliwa rais wa Chechnia mwaka 1997,lakini alipinduliwa miaka 2 baadae.Moscow imemlaumu Maskhadov kwa idadi fulani ya mashambulio yaliofanywa dhidi ya vikosi vya Russia katika eneo hilo.Amelaumiwa pia kwa utekajinyara wa watoto wa shule Septemba mwaka jana mjini Beslan,ambapo zaidi ya watu 300 walipoteza maisha yao na vile vile kwa utekaji nyara wa watu katika ukumbi wa michezo ya kuigiza mjini Moscow mwaka 2002 ambapo zaidi ya watu 100 waliuawa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW