1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Moto wauwawa 28 kwenye nyumba ya wazee

5 Novemba 2007

Takriban watu 28 wamekufa katika moto kwenye nyumba ya matunzo ya wazee nchini Urusi na maafisa wanawalumu wasimamizi wa nyumba hiyo kwa kuwashinda kuwahamisha wakaazi kwa wakati.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya masuala ya dharura ya Urusi Viktor Beltsov askari wa zima moto wamechelewa mno kupata taarifa za moto huo kwa sababu wafanyakazi wa nyumba hiyo kwa sababu fulani walisubiri kwa dakika 30 kabla ya kuwaarifu.

Moto huo ulizuka hapo jana karibu na mji wa Tula kilomita 200 kusini mwa Moscow.Watu 200 walikuwa wanaishi kwenye nyumba hiyo.

Maafa hayo ni mfululizo wa majanga ya moto nchini Urusi ambapo taasisi za taifa mara nyingi zimekuwa zikishutumiwa kwa usimamizi mbaya na kutotiliwa maanani vya kutosha kwa taratibu na zana za usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW