1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Putin aamuru wanamgambo wauwawe

13 Oktoba 2005

Rais wa Russia Vladamir Putin amewaamuru walinda usalama kuwapiga risasi wanamgambo wa Chechnya wanaoendeleza mapigano na polisi katika mji wa Nalchik, kusini mwa nchini hiyo.

Naibu wa waziri wa mambo ya ndani, Alexander Chekalin, amesema rais Putin hataki mtu yeyote mwenye bunduki kutoka mjini humo, na wale wanaotumia silaha kuwashambulia polisi lazima waangamizwe. Wanamgambo hao wamekivamia kituo cha polisi na majengo ya serikali katika harakati inayotilia shaka matamshi ya ikulu ya Kremlin kwamba imefaulu kulidhibiti eneo la Caucasus.

Wanamgambo wasiopungua 50 na maofisa 10 wa usalama wameuwawa na wengine zaidi ya 40 wakajeruhiwa katika mapigano hayo. Duru za polisi zinasema mapigano hayo yanafanyika kwenye majengo kadhaa ya serikali na shule. Wanafunzi wote wamehamishwa kutoka shule hiyo na maofisa wa usalama wamefaulu kuzuia shambulio dhidi ya uwanja wa ndege katika eneo la Karbadino-Balkariya.

Juhudi zinafanywa kuwaokoa mateka wa rehani wanaozuiliwa na wanamgambo hao. Mji wa Nalchik umefungwa na hakuna anayeruhusiwa kuingia ndani wala kutoka nje ya mji huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW