1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Russia kuanza mradi wa nyuklia na Iran

3 Novemba 2005

Russia inafanya mazungumzo na Iran kuanzisha mradi wa pamoja na Iran katika miaka michache ijayo. Maofisa wanasema mradi huo huenda ukawa suluhisho kwa mzozo wa nyuklia wa Iran.

Afisa mmoja katika shirika la nishati ya atomiki nchini Russia, amesema chini ya mpango huo, Russia na Iran zitarutubisha madini ya uranium na kuyauza duniani kote na kugawa faida nusu kwa nusu.

Ikiwa mpango huo utafaulu, itachukua miaka mingi kuuanzisha, lakini Russia inaamini utaleta faida kubwa. Hata hivyo pande zote ikiwemo Iran na umoja wa Ulaya lazima zikubali.

Afisa wa umoja wa Ulaya anayeshughulika na swala la Iran amesema Iran haitakuwa na hisa katika umilikaji wa teknolojia ya kurutubisha madini hayo katika mradi huo wa Russia, lakini wafanyikazi wake watapata ujuzi katika shughuli hiyo.