Moscow: Russia yatuma rambirambi Italia
13 Novemba 2003Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Russia Igor Ivanov amemtaka waziri mwenzake wa Italia Franco Frattini apokee rambirambi za Moscow kuhusu mripuko wa bomu uliowaua Wataliani 18 kwa uchache nchini Iraq, ilisema wiazara ya mambo ya nje hii leo. Baraza la mawaziri la Italia, leo limethibitisha kwamba Roma itavibakisha vikosi vyake nchini Iraq licha ya kutokea maujai ya Wataliani 18 hiyo jana, ilisema duru ya kisiasa. Baada ya kutokea shambulizi la bomu katika kituo cha wanajeshi wa Italia kusini mwa Iraq hiyo jana, Waziri Mkuu Silvio Berlusconi aliliambia Baraza la Senate kwamba Italia itawabakisha askari wake nchini humo.