1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Russia yaunga mkono juhudi za Ujerumani kuwa na kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

4 Julai 2005

Russia imesema kuwa inaunga mkono nia ya Ujerumani ya kupata kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa .

Haya yamethibitishwa na rais wa Russia Vladimir Putin katika mkutano alioufanya pamoja na kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder na rais wa Ufaransa Jacques Chirac jana Jumapili.

Viongozi hao watatu pia wamejadili kuhusu mkutano unaokuja wa kundi la mataifa yenye viwanda vingi G8 nchini Scotland pamoja na suala la mpango wa kinuklia wa Iran.

Mazungumzo hayo yalifanyika katika mji wa Kaliningrad nchini Russia, mji ambao unaadhimisha miaka 750 mwishoni mwa wiki hii.

Kwa muda wa karne kadha mji huo ulikuwa unajulikana kwa jina la Kijerumani la Königsberg.

Baada ya vita vikuu vya pili vya dunia , mji huo wa bandari katika eneo la Baltic ukawa sehemu ya Urusi ya zamani na wakaazi wa mji huo waliokuwa wakizungumza Kijerumani walifukuzwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW