MOSCOW: Schroeder,Bush wamewasili Moscow
9 Mei 2005
Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amewasili Moscow kuhudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya kumalizika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia barani Ulaya.Schroeder katika matamko yaliochapishwa siku ya jumamosi,kwenye magazeti ya Russia,ameomba msamaha kwa watu wa Russia kwa mateso yaliosababishwa na ushari wa Ujerumani ya Manazi.Akasema kualikwa kwake kushiriki katika sherehe za jumatatu ni ishara ya imani ya Russia kwa Ujerumani.Rais George W.Bush wa Marekani pia amewasili mjini Moscow kuhudhuria sherehe hizo.Bush amekutana na Rais wa Russia Vladimir Putin kwa majadiliano yaliohusika na mgogoro wa Israel na Wapalestina.Takriban viongozi 60 kutoka nchi mbali mbali wanatazamiwa kuhudhuria sherehe za kumbukumbu zitakazofanywa kwenye Uwanja Mwekundu mjini Moscow.