1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Seneti lapiga kura kuiondoa Russia katika mkataba wa Ulaya.

17 Novemba 2007

Baraza la seneti la Russia limepiga kura kusitisha ushiriki wa nchi hiyo katika mkataba muhimu unaotaka kupunguza idadi ya majeshi katika bara la Ulaya. Kura hiyo ambayo ilikuwa kwa kauli moja , ianfuatia uamuzi wa wiki iliyopita katika baraza la wawakilishi , Duma kusitisha ushiriki wa Russia katika mkataba huo wa kupunguza majeshi katika bara la Ulaya kuanzia Desemba 12. Hatua hiyo imeshutumiwa vikali na mataifa ya magharibi na NATO. Wakati huo huo shirika linaloangalia chaguzi katika bara la Ulaya OSCE limesema kuwa limeacha mipango yake ya kuangalia uchaguzi wa bunge nchini Russia utakaofanyika hapo Desemba 2 . Serikali za mataifa ya magharibi zimeishutumu Russia kwa kuweka idadi maalum ya watu watakaoangalia uchaguzi huo na kuweka vikwazo vya kiutendaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW