1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW :Wenye ukimwi wabaguliwa

15 Julai 2005

Wanawake wenye ukimwi pamoja na watoto wao wanabaguliwa na kunyanyaswa nchini Urusi,taarifa iliyotolewa na jopo la watetea haki za binadamu imesema hayo na kueleza kwamba ubaguzi huo aghalabu unafanywa na wahudumu wa afya.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi,wanawake wenye ukimwi karibu alfu 10 wamekuwa wanazaa nchini Urusi tokea mwaka wa 1997.Asilimia 20 ya akina mama hao wamewatelekeza watoto wao.

Taarifa hiyo imewakariri baadhi ya wanawake hao wakisema kwamba wanatukanwa na madaktari na wakati wakati mwingine wanakataliwa matibabu.

,
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW