SiasaAsia
Moscow yaishutumu Washington 'kuharibu' mkataba wa silaha
1 Februari 2023Matangazo
Msemaji wa serikali ya Urusi, Dmitry Peskov, amewaambia waandishi wa habari kwamba wanaamini muendelezo wa mkataba huo ni muhimu sana.
Ameongeza kuwa kwa upande mwingine wanaona Marekani imeharibu mfumo wa kisheria kwenye uwanja wa mapambano na usalama.
Mapema leo, balozi wa Urusi nchini Marekani alisema Urusi imekuwa ikiheshimu makubaliano hayo na inaendelea kufany ahivyo.
Mvutano kati ya nchi hizo mbili tayari ulikuwa umefikia hali mbaya, na hatua ya Urusi kuivamia Ukraine mnamo Februari mwaka uliopita ulizidisha mvutano huo.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani iliishutumu Urusi kwa kusimamisha ukaguzi na pia kufuta mazungumzo.
Lakini wizara hiyo haikuishutumu Urusi kwa kuongeza idadi ya vichwa vya nyuklia kupita kiwango kilichokubaliwa.