Moscow yaonya nchi za Magharibi kuhusu maafisa wake
29 Novemba 2023Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov, anayekabiliwa na vikwazo vya Ulaya, alilazimika kuombaruhusa ya kurukakatika anga ya Umoja wa Ulaya ili kuhudhuria mkutano huo wa siku mbili, ambao umeanza leo katika mji mkuu wa Macedonia ya Kaskazini, Skopje.
Soma pia:Mwanadiplomasia mkuu wa Latvia ataka nafasi ya juu NATO, akiahidi maono ya wazi kuhusu Urusi
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova amesema kuna juhudi za baadhi ya nchi za Magharibi kufanya kila liwezekanalo kuzuia ushiriki wa kawaida wa Urusi katika mkutano huo wa usalama.
Ukraine na mataifa ya eneo la Baltiki wamesema watasusia mkutano huo kama Lavrov atahudhuria, wakihoji kuwa Urusi inapaswa kutengwa kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema atahudhuria mkutano huo wa Skopje, lakini hatokutana moja kwa moja na Lavrov.